sw_exo_text_reg/18/01.txt

1 line
520 B
Plaintext

\c 18 \v 1 Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wake Musa, alisikia yote Mungu aliyofanya kwa Musa na kwa Israeli watu wake. Alisikia Yahweh ametoa Israeli kutoka Misri. \v 2 Yethro, baba mkwe wake Musa, akamchukua Zipora, mke wa Musa, baada ya kumpeleka nyumbani, \v 3 na wana wake wawili; jina mmoja lilikuwa Gershomu, kwa kuwa Musa alisema, "Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni." \v 4 Jina la mwingine lilikuwa Eliezeri, kwa kuwa Musa alisema, "Mungu wa babu yangu alikuwa msaada wangu. Aliniokoa na mkono wa Farao."