1 line
433 B
Plaintext
1 line
433 B
Plaintext
\v 12 Kisha twaa baadhi ya damu ya ng’ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu. \v 13 Kisha chukua mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu. \v 14 Lakini nyama yake huyo ng’ombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya marango; ni sadaka kwa ajili ya dhambi. |