sw_est_text_reg/04/01.txt

1 line
435 B
Plaintext

\c 4 \v 1 Modeka aliposikia kilichokuwa kimepangwa dhidi yao, alirarua mavazi yake na kuvaa magunia na majivu. Akaenda katikati mwa mji na kulia kwa sauti na uchungu mwingi. \v 2 Akaenda hadi langoni mwa mfalme; kwa sababu hakuna aliye ruhusiwa kuingia akiwa amevaa magunia. \v 3 Amri hii ilipofika katika kila jimbo, kulikuwa na kilio kikubwa kwa Wayahudi, na kufunga, kulia na maombolezo. Wengi wao walilala katika magunia na majivu.