\v 1 Kisha Mfalme Ahusiero akaweka kodi juu ya nchi na maeneo ya bahari. \v 2 Mafanikio yote na nguvu na ukuu wake, pamoja na wa Modekai ambao mfalme alimwinua, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu ya wafalme wa Wamedi na Waajemi.