sw_est_text_reg/02/08.txt

1 line
486 B
Plaintext

\v 8 Wasichana wengi waliletwa ikulu Shushani, baada ya tangazo na amri ya mfalme kutolewa. Waliwekwa chini ya usimamizi wa Hegai. Esta naye alikuwa ni miongoni mwa wasichana walioletwa na kuwekwa chini ya usimamizi wa Hegai, mwangalizi wa wanawake. \v 9 Esta alimfurahisha, na akapata kibali mbele ya Hegai. Akampa vipodozi na sehemu ya chakula. Akampa wahudumu wa kike saba kutoka katika ikulu ya mfalme, na akampeleka na wahudumu wa kike katika sehemu bora katika nyumba ya wanawake.