sw_est_text_reg/01/05.txt

1 line
532 B
Plaintext

\v 5 Siku hizi zilipotimia, Mfalme aliaandaa karamu iliyodumu kwa siku saba. Karamu hii ilikuwa kwa watu wote walioishi katika ikulu ya Shushani, tangu mkubwa hadi mdogo. Behewa la bustani ya ikulu ya mfalme ndiyo karamu ilipofanyikia. \v 6 Behewa la bustani lilipambwa kwa mapazia meupe ya pamba na urujuani, yalifungwa kwa kamba za kitani safi na zambarau, yakiwa yametundikwa kwa pete za fedha na nguzo za marimari. Kulikuwa na makochi ya dhahabu na fedha juu ya sakafu ya marimari, mawe mekundu na meupe, na ya manjano na meusi.