sw_est_text_reg/08/10.txt

1 line
603 B
Plaintext

\v 10 Modekai akaandika kwa jina la Mfalme Ahusiero na akazipiga muhuri kwa pete ya mfalme. Akapeleka nyaraka kwa matarishi, akawapandisha kwenye farasi waendao kwa haraka waliotumika kwa huduma ya mfalme, waliozaliwa kwa mfalme. \v 11 Mfalme akawapa Wayahudi wote katika majimbo ya utawala wake kibali cha kukusanyika ,na kujilinda, na ruhusa ya kuangamiza, kuua na kuharibu mtu yeyote aliyekuwa na kusudi la kuwaua Wayahudi wote na kupora mali zao. \v 12 Jambo hili lilipaswa litekelezwe katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ambao ni mwezi wa Adari.