sw_est_text_reg/02/01.txt

1 line
289 B
Plaintext

\c 2 \v 1 Baada ya mambo haya, na hasira ya mfalme Ahusiero kutulia, alifikiri kuhusu Malkia Vashiti na alichokuwa amekifanya na tangazo alilokuwa ameamuru litolewe ya Vashiti kupoteza sifa za kuwa malkia. \v 2 Kisha vijana waliomtumikia mfalme wakasema, mfalme atafutiwe mabikira warembo.