sw_deu_text_reg/23/12.txt

1 line
465 B
Plaintext

\v 12 Pia unatakiwa kuwa na eneo nje ya kambi ambayo utakwenda; \v 13 na utakuwa na kitu katika zana zako cha kuchimbia; utakapochuchumaa kujisaidia, unapaswa kuchimbia nacho na kisha kurudishia udongo na kufunika kile kilichotoka kwako. \v 14 Kwa maana Yahwe Mungu wako anatembea miongoni mwa kambi yenu kuwapa ushindi na kuwapa maadui zenu mkononi mwenu. Kwa hiyo kambi yenu lazima iwe takatifu, ili kwamba asione kitu chochote kichafu miongoni mwenu na kuwaacha.