sw_deu_text_reg/34/01.txt

1 line
369 B
Plaintext

\v 1 Musa aliondoka kutoka nyanda za Moabu mpaka mlima wa Nebo, hadi kilele cha Pisga, kilicho mkabala na Yericho. Huko Yahwe alimwonyesha nchi yote ya Gileadi kutoka umbali wa Dani, \v 2 na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi, \v 3 na Negevi, na uwanda wa bonde la Yericho, mji wa mitende, mpaka umbali wa Soari.