sw_deu_text_reg/21/10.txt

1 line
343 B
Plaintext

\v 10 Utakapokwenda kupigana vita dhidi ya maadui zako na Yahwe Mungu wako atakapokupa ushindi na kuwaweka chini ya mamlaka yako, na ukawachukua mbali kuwa mateka, \v 11 kama kati ya mateka ukamwona mwanamke mzuri, nawe ukamtamani na kutaka kujitwalia awe mke wako, \v 12 basi utamleta nyumbani kwako; atanyoa nywele zake na kukata kucha zake.