sw_deu_text_reg/19/08.txt

1 line
534 B
Plaintext

\v 8 Kama Yahwe Mungu wenu apanua mipaka yenu, kama alivyoapa kwa mababu zenu kufanya, na kuwapa nchi yote ambayo amewaahadia kuwapa mababu zenu; \v 9 kama mnazishika amri hizi zote kuzifanya, ambazo ninakuamuru leo- amri za kumpenda Yahwe Mungu wenu na daima kutembea katika njia zake, basi mnapaswa kuongeza miji mitatu zaidi kwa ajili yenu, isipokuwa ile mitatu. \v 10 Fanya hivi ili kwamba damu isiyo na hatia isimwagwe katikati ya nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa kwa ajili ya urithi, ili kwamba pasiwepo hatia ya damu kwenu.