sw_deu_text_reg/19/01.txt

1 line
470 B
Plaintext

\v 1 Wakati Yahwe Mungu wenu anayafutilia mbali mataifa, yale ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa nchi yao, na wakati mnakuja kwao na kuishi katika miji yao na nyumba, \v 2 mnapaswa kuchagua miji mitatu kwa ajili yenu katikati mwa nchi yenu ambayo Yahwe Mungu anawapa kuimiliki. \v 3 Mnapaswa kujenga barabara na kugawa mipaka ya nchi yenu katika maeneo matatu, nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anafanya kuimiliki, ili kwamba kila mmoja anayeua mtu mwingine apate kukimbia hapo.