sw_deu_text_reg/13/01.txt

1 line
406 B
Plaintext

\v 1 Kama miongoni mwenu ainuka nabii au muota ndoto, \v 2 na kama anawapa ishara au maajabu, na kama ishara au maajabu yanatokea, kama alivyozungumza kwenu na kusema, " Ebu tuifuate miungu mingine, ambayo hatuijui, na tuiabudu. \v 3 Usisikilize maneno ya nabii huyo, au kwa huyo muota ndoto, kwa kuwa Yahwe Mungu wako anakujaribu kujua kama unampenda Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na roho yako yote.