sw_deu_text_reg/04/44.txt

1 line
397 B
Plaintext

\v 44 Hii ni sheria ambayo Musa aliweka mbele ya watu wa Israeli, \v 45 hizi ni amri za agano, sheria, na amri zingine alizungumza na watu wa Israeli wakati walipotoka Misri, \v 46 pindi walikuwa Mashariki mwa Yordani, katika bonde mkabala wa Beth Peori, katika nchi ya Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyewahi kuishi Heshbon, ambaye Musa na watu wa Israeli waliwahi kumshinda wakati walipotoka Misri.