\v 1 Vitu hivi vitakavyokuja juu yako, baraka na laana nilizoziweka mbele yako, na utakapozirejea akilini miongoni mwa mataifa mengine ambapo Yahwe Mungu wako kawapeleka, \v 2 na utakapomrudia Yahwe Mungu wako na kutii sauti yake, na kufuata yote ambayo nayokuamuru leo – wewe na watoto wako – kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote, \v 3 kisha Yahwe Mungu wako atageuza kutekwa kwako na kukuhurumia; atawarudisha na kuwakusanya kutoka kwa watu wote ambapo Yahwe Mungu wako aliwatawanya.