\v 2 Wakati unakaribia kuingia kwenye vita, kuhani anapaswa kuwasogelea na kuongea na watu. \v 3 Anapaswa kuwaambia,"Sikilizeni, Israel, mnaenda kupigana dhidi ya maadui zenu. Msidhofishe moyo wenu. Msiohofu au kutetemeka. Msiwaogope. \v 4 Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ndiye aendae pamoja nanyi kupigana kwa ajili yenu dhidi ya maadui zenu na kuwaokoa.