\v 15 Hata hivyo, mtaweza kuua na kula wanyama ndani ya malango yenu, kama mnavyotaka, kupokea baraka ya Yahwe Mungu wenu kwa ajili ya yote amewapa; na watu wasio wasafi na wasafi wote wanaweza kula, wanyama kama vile paa na kulungu. \v 16 Lakini hamtakula damu, mtaimwaga kwenye ardhi kama maji.