Sun Jun 26 2022 22:15:36 GMT+0300 (East Africa Time)

This commit is contained in:
tsDesktop 2022-06-26 22:16:06 +03:00
commit 37a340f3f2
483 changed files with 549 additions and 0 deletions

1
01/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Haya ni maneno ambayo Musa aliyasema kwa Israeli wote ng'ambo ya jangwa la Yordani, katika tambarare ya mto wa Yordani juu ya Suph, katikati mwa Paran, Topheli, Laban, Hazeroth, na Di Zahab. \v 2 Ni safari ya siku kumi na moja toka Horabu kupitia njia ya mlima wa Seir kwenda Kadeshi Barnea.

1
01/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Ilitokea kwenye mwaka wa nne, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa alizungumza kwa watu wa Israeli, kuambia yote yale Yahwe aliyomwamuru kuhusu wao. \v 4 Hii ilikuwa baada ya Yahwe kumvamia Sihoni mfalme wa Amoria, ambaye aliishi huko Heshboni, na Ogi mfalme wa Bashani, ambaye aliishi huko Ashtarothi ya Edrei.

1
01/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Ng'ambo ya Yordani, katika nchi ya Moabu, Musa alianza kutangaza maelekezo haya, akisema, \v 6 "Yahwe Mungu wetu alisema nasi huko Horebu, akisema, umeishi vya kutosha katika milima ya nchi hii.

1
01/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Geuka na uanze safari yako, na uende kwenye nchi ya milima ya Amorites, na kwenye maeneo yote karibu na tambarare ya mto Yordani, katika nchi ya milima, na nyanda za chini, huko Negev, na pwani - nchi ya Wakanani na huko Lebanoni mbali ya mto mkuu wa Euphratesi. \v 8 Tazama, nimetenga nchi kwa ajili yako, nenda ndani na umiliki nchi ambayo Yahwe aliapa kwa baba zako, Ibrahimu, Isaka na Yakobo, kuwapa na uzao wao baada yao.

1
01/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Nilisema nawe kwa wakati huo, nikisema, siwezi nikakubeba peke yangu, \v 10 Yahwe Mungu wako amekuzidisha, na tazama, leo umekuwa umati wa nyota angani. \v 11 Yahwe aweza, Mungu wa baba zako, kukufanya wewe mara elfu moja zaidi ya ulivyo, na kukubariki, kama alivyokuahidi!

1
01/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Lakini inawezekanaje mimi peke yangu kubeba shehena zako, mizigo yako, na migogoro yako? \v 13 Chukua wanaume wa hekima, wanaume waelewa, na wanaume walio na sifa nzuri toka kila kabila, nitawafaya kuwa vichwa juu yenu. \v 14 Mlinijibu na kusema, 'Jambo ulilolisema ni zuri kwetu kufanya.'

1
01/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Kwa hiyo nilichukua vichwa vya makabila yenu, wanaume wa hekima, na wanaume wenye sifa nzuri, na nikawafanya kuwa vichwa juu yenu, jemedari kwa elfu, jemedari kwa hamsini, jemedari kwa kumi, na maakida, kabila kwa kabila. \v 16 Niliwaamuru waamuzi wenu kwa wakati huo, kusema, 'Zikiliza mabishano kati ya ndugu zenu, na muhukumu ya haki kati ya ndugu na ndugu zake, na mgeni aliye pamoja naye.

1
01/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Hamtaonesha upendeleo kwa yeyote katika mgogoro, mtasikia madogo na makubwa pia. Hamtaogopa uso wa mtu, kwa kuwa hukumu ni ya Mungu. Migogoro iliyo migumu kwenu, mtaniletea mimi, na mimi nitaisikiliza. \v 18 Niliwaamuru kwa wakati huo mambo yote mtakayofanya.

1
01/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Tulisafiri toka Horebu na kwenda kupitia jangwa lile kubwa lote na lenye kutisha lile mliloliona, katika njia yetu kuelekea nchi ya milima huko Amorites, kama Yahwe Mungu wetu alivyotuamuru sisi, na tukaja Kadeshi ya Barnea.

1
01/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Niliwambia, mmekuja kwenye nchi ya milima ya Amorites, ambayo Yahwe Mungu wetu anatupa sisi. \v 21 Tazama, Yahwe Mungu wenu amekwisha weka nchi mbele yenu; nenda juu, muimiliki, kama Yahwe, Mungu wa baba zenu, amekwisha zungumza nanyi, msiogope wala kukata tamaa.

1
01/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Kila moja wenu alikuja kwangu na kusema, 'Basi tutume watu mbele yetu, ili kwamba waweze kupepeleza nchi kwa ajili yetu, na kutuletea sisi neno kuhusiana na njia ya wapi tuvamie, na kuhusiana na miji tutakayoingia. \v 23 Shauri hilo lilinibariki mimi, 'Nilichukua watu kumi na mbili kutoka kwenu, mtu moja kwa kila kabila. \v 24 Waligeuka na kwenda juu ya nchi ya milima, kufika kwenye bonde la Eshcol na kufanya upepelezi wa kina.

1
01/25.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 25 Walichukua baadhi ya mazao ya ardhi mikononi mwao na kuleta kwetu, Pia walileta neno na kusema, 'Ni nchi nzuri ambayo Yahweh Mungu wetu anatupa sisi'

1
01/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Bado mlikataa kushambulia, lakini mliasi dhidi ya amri ya Yahwe Mungu wenu. \v 27 Mlilalamika katika mahema yenu na kusema, "Ni kwa sababu Yahwe alituchukia sisi kwa kuwa ametutoa katika nchi ya Misri, kuteweka katika mikono ya Amorites kutuangamiza. \v 28 Tuende wapi sasa? Ndugu zetu wamefanya mioyo yetu kuyeyuka, kusema, Hao watu ni wakubwa na warefu zaidi yetu, miji yao ni mikubwa na imeimarishwa kwenda mbinguni; zaidi ya yote, tumewaona wana wa Anakim huko"

1
01/29.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 29 Kisha nikasema nao, msitishwe wala msiwaogope. \v 30 Yahwe Mungu wenu, ambaye aenda mbele yenu, atawapigania, kama yote aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu, \v 31 na pia katika jangwa, ambapo mmekwisha muona Yahwe Mungu wenu jinsi alivyowabeba, kama mtu abebavyo mtoto wake, kokote mlikoenda mpaka kufika hapa.'

1
01/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 Bado licha ya neno hili hakumwamini Yahwe Mungu wenu, \v 33 aliyeenda mbele yenu kwenye njia kutafuta eneo kwa ajili yenu kuweka kambi, katika moto kwa usiku, katika mawingu kwa mchana.

1
01/34.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 34 Yahwe alisikia sauti ya maneno yenu na alikasirika; aliapa na kusema, \v 35 Hakika hakuna mmoja ya hawa watu wa kizazi hiki kiovu wataona nchi nzuri ambayo niliapa kuwapa babu zao, \v 36 kasoro Kalebu mwana wa Jephuneeh; yeye ataiona. Yeye nitampa nchi ambayo amekwisha kuikanyanga, na watoto wake, kwa sababu alimfuata Yahwe kwa ukamilifu.'

1
01/37.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 37 Pia Yahweh alinikasirikia mimi kwa sababu yenu, kusema, 'Wewe pia hautaingia huko, \v 38 Yoshua mwana wa Nuh, ambaye amesimama mbele yako, yeye ataingia, mtie moyo, kwani yeye atawaongoza Israeli kuimiliki.

1
01/39.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 39 Zaidi ya yote, watoto wenu wadogo, ambao mlisema watakuwa waathirika, ambao leo hawana elimu ya uzuri au ubaya-wataenda ndani huko. Wao nitawapa nchi hiyo, na wataimiliki. \v 40 Lakini ninyi, geuka na muuanza safari kwenda jangwani kwa kuambaa njia ya bahari ya mianzi'.

1
01/41.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 41 Kisha mlinijibu na kusema kwangu, 'Tumetenda dhambi dhidi ya Yahwe, tutaenda juu na kupigana, tutafuata yote ambayo Yahwe Mungu wetu ametuamuru sisi kufanya'. Kila mtu miongoni mwenu aliweka silaha za vita, na mlikuwa tayari kuvamia nchi ya milima. \v 42 Yahwe alisema nami, 'Waambie, msivamie na kupigana, kwa kuwa sitakuwa pamoja nanyi, na mtashindwa na adui zenu'.

1
01/43.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 43 Nilizungumza nanyi kwa njia hii, lakini hamkunisikiliza, Mliasi dhidi ya amri ya Yahwe, mlikuwa wenye kiburi na mlivamia nchi ya milima. \v 44 Lakini Amorites, ambayo waliishi katika nchi hiyo ya milima, walitoka dhidi yenu na kuwafukuza kama nyuki, na kuwapiga chini huko Seir, mbali kama Hormah.

1
01/45.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 45 Mlirudi na kulia mbele ya Yahwe; lakini Yahwe hakusikiliza sauti zenu, wala hakuwa makini kwenu. \v 46 Kwa hiyo mlibaki Kadeshi siku nyingi, siku zote mlibaki huko.

1
02/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kisha tuligeuka na kuanza safari kuelekea jangwani kwa njia ya Bahari ya Mianzi, kama Yahwe alivyosema nami, tulienda kuzunguka mlima wa Seir kwa siku nyingi. \v 2 Yahwe alizungumza nami, kusema, \v 3 Mmeuzungunga mlima huu kwa muda mrefu; geukeni kaskazini.

1
02/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Waamuru watu, kusema, "Mtapita kupitia mpaka wa ndugu zenu, wazao wa Esau, ambao wanaishi Seir; watawaogopa ninyi. Kwa hiyo muwe makini \v 5 msipigane nao, kwa kuwa sitawapa nchi yoyote yao, hapana, hakuna hata vya kutosheleza unyao wa mguu kukanyanga, kwa kuwa nimekwisha mpa Esau Mlima wa Seir kama miliki.

1
02/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Mtanunua chakula kutoka kwao kwa pesa, ili kwamba muweze kula, pia mtanunua maji kutoka kwao kwa pesa, ili kwamba muweze kunywa. Kwa kuwa \v 7 Yahwe Mungu wenu amewabariki katika kazi za mikono yenu, amejua kutembea kwenu kupitia jangwa hili kuu. Kwa hii miaka arobaini Yahwe Mungu wenu amekuwa pamoja nanyi, na hamjapungukiwa chochote.

1
02/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Basi tulipita karibu na ndugu zetu, wa wazao wa Esau, ambao wanaishi Seir, mbali na barabara la Arabah, kutoka Elathi, na kutoka Ezioni Geber. Na tuligeuka na kupita karibu na jangwa la Moabu.

1
02/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Yahweh aliniambia mimi,'Usiisumbue Moabu, na usipigane nao katika vita. Kwa kuwa sitakupa nchi yake kwa miliki yako, kwa sababu nimewapa Ar wazao wa Lot, kuwa miliki yao'.

1
02/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 (Hapo awali waliishi Waemi, watu kama wakuu, wengi, na warefu kama Waanaki; \v 11 hawa pia wanafikiriwa kuwa Rephaimu, kama Waanaki, lakini Wamoabi huwaita Waemi.

1
02/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Wahori pia waliishi hapo awali Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafuata. Waliwaharibu kutoka mbele yao na kuishi katika eneo lao, kama Israeli ilivyofanya kwa nchi ya umiliki wake ambayo Yahwe aliwapa.)

1
02/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 "Sasa inuka na uende kwenye kijito cha Zeredi". Kwa hiyo tulienda kwenye kijito cha Zeredi. \v 14 Sasa tangu siku ambapo tulikuja kutoka Kadesh Barnea mpaka tukavuka kijito cha Zeredi, ilikuwa miaka thelathini na nane. Ilikuwa kwa wakati huo kizazi chote cha watu waliofaa kupigana walikuwa wamekwisha ondoka kwa watu, kama Yahwe alivyokuwa ameapa kwao. \v 15 Zaidi ya yote, mkono wa Yahwe ulikuwa kinyume na kizazi hicho ili kuweza kuwaangamiza kutoka kwa watu mpaka walipoondoka.

1
02/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Basi ilitokea, wakati watu wote waliofaa kwa kupigana walikuwa wamekufa, na kutoweka miongoni mwa watu, \v 17 kwamba Yahwe alizungumza nami, kusema, \v 18 Leo mtavuka Ar, mpaka wa Moabu. \v 19 Wakati mtakapofika karibu na mkabala wa watu wa Ammoni, msiwasumbue au kupigana nao, kwa kuwa sitawapa nchi yoyote ya watu wa Ammoni kama miliki, kwa sababu nimekwisha wapa wazao wa Lutu kama miliki".

1
02/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 (Hiyo tena ilifikiriwa kuwa nchi ya Rephaimu. Warephaimu waliishi hapo awali-lakini Wammonites wanawaita Zamzummim, \v 21 watu kama wakuu, wengi, na warefu kama Anakim. Lakini Yahwe aliwaharibu mbele ya Wammonites na waliwafuata na kuishi katika maeneo yao. \v 22 Yahwe huyu pia alifanya kwa watu wa Esau ambao wanaishi Seiri, wakati alipowangamiza Wahori kutoka mbele yao, na wazao wa Esau waliwafuata na waliishi katika maeneno yao mpaka leo.

1
02/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Na Waavi, walioishi katika vijiji vya mbali ya Gaza, Wakaftori, ambao wanatokana na Kaftori, waliwangamiza na kuishi katika maeneo yao.)

1
02/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Sasa inuka, nenda njia yako na uvuke bonde la Arnoni, tazama, nimekupa mkononi mwako Sihoni ya Amorite, mfalme wa Heshboni, na nchi yake. Anza kuimiliki na pigana naye katika vita. \v 25 Leo nitaanza kuweka woga na hofu yenu kwa watu ambao wako chini ya anga lote, watasikia habari kuhusu ninyi na watatemeka na kuwa na shida kwa sababu yenu'.

1
02/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Nilituma wajumbe toka jangwa la Kedemothi kuelekea Sihoni, mfalme wa Heshbon, pamoja na maneno ya amani, kusema, \v 27 Hebu nipite katika nchi yako; nitapita kwenye barabara kuu, sitageuka mkono wa kulia wala kushoto.

1
02/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Mtaniuzia mimi chakula kwa pesa, ili kwamba niweze kula, nipe maji kwa pesa, ili kwamba niweze kunywa, peke niruhusu kupitia kwa miguu yangu, \v 29 kama wazao wa Esau wanaoishi Seiri, na Moabu wanaoishi Ari, walifanya kwangu, mpaka nivuke Yordani ndani ya nchi ambayo Yahwe Mungu wetu anatupa sisi'.

1
02/30.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 30 Lakini Sihon, mfalme wa Heshbon, asingeturuhusu kupitia kwake; kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ameifanya ngumu akili yake na kufanya moyo wake kuwa ukaidi, ili kwamba aweze kumshinda kwa nguvu zake, ambayo amekwisha kufanya leo. \v 31 Yahwe alisema kwangu, "tazama, Nimeanza kumuokoa Sihoni na nchi yake mbele yako; kuanza kuimiliki, ili kusudi muweze kumiliki nchi yake.

1
02/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 Kisha Sihon alikuja dhidi yetu, yeye na watu wote wake, kupigana huko Jahazi. \v 33 Yahwe Mungu wetu alimtoa kwetu na tulimshinda, tulimpiga mpaka kufa, watoto wake, na watu wake wote.

1
02/34.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 34 Tulichukua miji yake yote kwa wakati huo na kuharibu kabisa kila mji- wanaume na wanawake na watoto wadogo; hatukuacha aliyenusurika. \v 35 Ng'ombe peke tulichukua kama mateka kwa ajili yetu, sambamba na mateka ya miji tuliochukua.

1
02/36.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 36 Kutoka Aroer, ambayo iko kwenye ukingo wa bonde la Arnon, na kutoka kwenye mji ambao uko bondeni, yote kwa njia ya kuelekea Galeadi, hapakuwa na mji uliokuwa mrefu kwetu. Yahwe Mungu wetu alitupa ushindi dhidi ya maadui zetu mbele yetu. \v 37 Ilikuwa nchi ya wazao wa Ammoni peke yake ambayo hamkuingia, sambamba na sehemu zote za mto Jabboki, na miji ya nchi ya milima- popote pale Yahwe Mungu wetu ametukataza sisi kwenda.

1
03/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kisha tuligeuka na kwenda njia ya juu Bashani. Ogi, mfalme wa Bashani, alikuja na kutuvamia, yeye na watu wake wote, kupigana huko Edrei. \v 2 Yahwe aliniambia mimi, "Usimuogope; kwa kuwa nimekupa ushindi dhidi yake na nimewaweka watu wake wote na nchi yake chini ya utawala wako. Utamfanya kama ulivyomfanya Sihoni, mfalme wa Amorites, aliyeishi Heshbon.

1
03/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Kwa hiyo Yahwe Mungu wetu pia alitupa ushindi dhidi ya Ogi mfalme wa Bashani, na watu wake wote waliwekwa chini ya utawala wetu. Na tulimpiga mpaka kufa na hakuna yoyote wa watu wake walibaki. \v 4 Tulichukua miji yake yote kwa wakati huo; hapakuwa na mji hata mmoja ambao hatukuchukua kutoka kwao: miji sitini - mikoa ya Argobi yote, ufalme wa Ogi Bashani.

1
03/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Hii ilikuwa miji iliyoimarishwa na kuta ndevu, malango, na vizuizi, hii ilikuwa licha ya vijiji vingi sana vilivyokuwa havina kuta. \v 6 Tuliviangamiza kabisa, kama tulivyofanya kwa Sihoni mfalme wa Heshbon, kabisa tuliangamiza kila mji- wanaume na wanawake na watoto wadogo. \v 7 Lakini ng'ombe wote na mateka ya miji, tilichukua kama mateka wetu.

1
03/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Kwa wakati huo tulichukua nchi kutoka kwenye mkono wa wafalme wawili wa Amorites, waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani, kutoka kwenye bonde la Arnon kwenda mlima wa Hermoni, \v 9 (Mlima wa Hermoni, Wasidonia huita Sirioni, na Wamorites huita Seniri) \v 10 na miji yote ya tambarare, yote Gileadi, na yote Bashani kupita njia yote ya Salekah na Edrei, miji ya ufalme wa Ogi huko Bashani".

1
03/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 (Kwa mabaki ya Refaimu, mfalme Ogi pekee wa Bashani alikuwa amebaki. Tazama! Kitanda chake kilikuwa cha chuma. Hakuna huko Rabbah, ambako wazao wa Ammoni waliishi? Ilikuwa dhiraa tisa urefu na dhiraa nne upana, hiyo njia walitumia watu kupima.)

1
03/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 "Hili eneo ambalo tulichukua kumiliki kwa wakati huo-kutoka Aroer, kwamba ni kwa bonde la Arnon, na nusu ya nchi ya mlima wa Gileadi, na miji yake-Nilimpa Reubenites na kwa Gadites. \v 13 Waliobaki wa Gileadi na Bashani yote, ufalme wa Ogi, Niliwapa nusu kabila la Manasseh: kwa wote wa Argob, na Bashani yote. (Eneo hilo linaitwa nchi ya Refaim)

1
03/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Jair, mzao wa Manasseh, alichukuwa mkoa wote wa Argob, kuelekea mpaka wa Geshunites na wa Maacathites. Aliita mkoa hata Bashani kwa jina lake, Havvothi Jair, hadi leo.)

1
03/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Nilimpa Gileadi kwa Machir. \v 16 Kwa Reubenites na kwa Gadites nilitoa eneo kutoka kwa Gileadi kuelekea bonde la Arnon- katikati mwa bonde ni mpaka wa eneo- na kuelekea mto wa Jabbok, ambao umepakana ni wazao wa Ammoni.

1
03/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Moja ya mipaka mingine pia ni tambarare ya bonde la mto wa Yordani, kutoka Chinnerethi kuelekea bahari ya Arabah(ambayo ni bahari ya Chumvi) kuelekea miteremko wa mlima wa Pisgah mashariki.

1
03/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Nilikuamuru wewe kwa wakati huo, kusema, Yahwe Mungu wako amekupa nchi hii kuimiliki, wewe, wamaume wote wa vita, watapita wakiwa na silaha mbele ya ndugu zako, watu wa Israeli.

1
03/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Lakini wake zenu, watoto wenu, na ng'ombe zenu (najua ya kuwa una ng'ombe wengi) watabaki katika miji yenu niliyowapa, \v 20 mpaka Yahwe awape pumziko ndugu zenu, kama alivyo kwenu, mpaka wamiliki pia nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa ng'ambo ya pili Yordani, kisha mtageuka, kila mtu wenu, kwa mali zenu ambazo nimekwishawapa.

1
03/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Nilimwamuru Yoshua kwa wakati huo, kusema, 'Macho yenu yameona yote yale Yahwe Mungu wenu amefanya kwa hawa wafalme wawili; Yahwe atafanya hivyo kwa falme zote kote mtakakoenda. \v 22 Hamtawaogopa, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ndiye atakaoawapigania.'

1
03/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Nilimsihi Yahwe kwa wakati huo, kusema, \v 24 'O Bwana Yahwe, umeanza kumuonesha mtumwa wako ukuu wako na mkono wako wa hodari; kwa kuwa nani mungu aliyeko huko mbinguni au duniani ambaye anaweza kufanya kazi zilezile kama ilivyofanya, na matendo yaleyale makuu? \v 25 Hebu niende juu, Ninakuoma, na nione nchi nzuri ambayo ng'ambo ya pili ya Yordani, ile nchi nzuri ya mlima, na pia Lebanoni.

1
03/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Lakini Yahwe alikuwa amenikasirikia mimi kwa sababu yenu, hakunisikiliza mimi. Yahwe alisema kwangu, "Hebu hii iwe ya kutosha kwako - usizungumze zaidi tena kwangu kuhusu jambo hili. \v 27 nenda juu ya kilele cha Pisgah na uinue macho yako magharibi, mashariki, kusini na mashariki; tazama kwa macho yako kwa kuwa hautaenda zaidi ya Yordani.

1
03/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Badala yake, mwelekeze Yoshua na kumtia moyo na kumuimarisha, kwa kuwa ataenda zaidi mbele ya watu, na atawasababisha kuirithi nchi ambayo mtaiona. \v 29 Kwa hiyo tulibaki katika bonde mkabala mwa Beth Peor.

1
04/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Sasa, Israeli, sikiliza sheria na amri ambayo niko karibu kukufundisha, kuzifanya, ili kwamba uweze kuishi na kuingia ndani na kumiliki nchi ambayo Yahwe, Mungu wa baba zako, anakupa. \v 2 Hautaongeza maneno ambayo nakuamuru, wala hautayapunguza, ili kwamba uweze kushika amri ya Yahwe Mungu wako ambazo naenda kukuamuru.

1
04/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Macho yako yamekwisha ona nini Yahwe alifanya kwa sababu ya Baal Peor, kwa kuwa watu wote waliomfuata Baali Peor, Yahwe Mungu wenu amekwisha kuwaangamiza kutoka miongoni mwenu. \v 4 Lakini walioambatana na Yahwe Mungu wenu wako hai leo, kila moja wenu.

1
04/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Tazama, nimewafundisha sheria na amri, kama Yahwe Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ila kwamba mfanye hivyo katikati mwa nchi ambayo mnaiendea ili kusudi muimiliki. \v 6 Kwa hiyo washikilieni na kuwafanya, kwa kuwa hii ni hekima yenu na uelewa wenu mbele ya macho ya watu watakaosikia amri hizi zote na kusema, "Hakika taifa hili kubwa lina watu wa hekima na uelewa.'

1
04/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Kuna taifa gani jingine la vile liko hapo lina mungu karibu nao, kama Yahwe Mungu wetu tunapomwita wakati wowote? \v 8 Kuna taifa kubwa gani jingine liko hapo ambalo lina sheria na amri ili kwamba haki pamoja na sheria ambayo ninaweka mbele yenu leo?

1
04/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Zingatia peke na kuwa makini kujilinda, ili usisahau mambo ambayo macho yako yameona, ili kwamba yasiuwache moyo wako kwa siku zote za maisha yako. Badala yake, yafanye yajulikane kwa watoto wako na wana watoto wako. \v 10 Kuhusu siku ile uliyosimama mbele ya Yahwe Mungu wako katika Horeb, wakati Yahwe alisema nami, 'Nikusanyie watu, na nitawafanya wasikia maneno yangu, ili kwamba waweze kujifunza kuniogopa mimi siku zote ambazo wanazoishi duniani, na kwamba waweze kuwafundisha watoto wao.

1
04/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Mlikuja karibu na kusimama katika wayo wa mlima. Mlima uliwaka moto kwenye moyo wa mbinguni, pamoja na giza, mawingu na giza jembamba. \v 12 Yahwe alizungumza katikati ya moto, ulisikia suati pamoja na maneno yake, lakini hakuona umbo, ila ulisikia sauti peke.

1
04/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Alitangaza kwenu agano lake ambalo aliwaamuru ninyi kulifanya, amri kumi. Aliziandika kwenye vibao viwili vya mawe. \v 14 Yahwe aliniamuru mimi kwa wakati huo kuwafundisha sheria na amri, ili kwamba muweze kuzifanya katika nchi mnaoivuka kwenda kuimiliki.

1
04/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Basi iweni waangalifu ninyi wenyewe - kwa kuwa mliona hakuna namna ya umbo siku hiyo ambapo Yahweh alizungumza nanyi huko Horeb kutoka katikati mwa moto, \v 16 ili kwamba usiharibike na kuchonga umbo katika sura ya kiumbe chochote, umbo la mwanaume au mtu wa kike, \v 17 au sura ya mnyama aliye katika nchi, au sura ya ndege yoyote wa mabawa arukae katika anga, au \v 18 sura ya kitu chochote kitambaacho katika ardhi, au sura ya samaki yoyote katika maji chini ya ardhi.

1
04/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Hautainua macho yako juu mbinguni na kutazama jua, mwezi, au nyota - jeshi lote la mbinguni- ukusogezwa na kuviabudu na kuvisujudia- vile vyote ambavyo Yahwe Mungu wenu amewapa hisa watu wote walio chini ya anga lote. \v 20 Lakini Yahwe amewatoa ninyi na kuwaleta nje ya tanuru la chuma, nje ya Misri, kuwa kwake watu wa urithi wake, kama mlivyo leo.

1
04/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Yahwe alinikasirikia mimi kwa sababu yenu; aliapa kwamba nisiende ng'ambo ya Yordani, na kwamba nisiende kwenye nchi nzuri, nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa ninyi kama urithi. \v 22 Badala yake, ninapaswa kufa katika nchi hii, sipaswi kwenda ng'ambo ya Yordani, lakini mtaenda ng'ambo na kuimiliki nchi nzuri

1
04/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Zingatia ninyi wenyewe, ili kwamba msisahau agano la Yahwe Mungu wenu, alilolifanya pamoja nanyi, na kujichongea mfano wa sanamu katika uombo la kitu chochote ambacho Yahwe Mungu wenu amewakataza kufanya. \v 24 Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ni moto ulao, Mungu wa wivu.

1
04/25.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 25 Wakati mnapozaa watoto na wana watoto, na wakati mtakapo kuwa katika nchi kwa muda mrefu, na kama mtaharibikiwa ninyi na kuchonga umbo la umbo lolote, na kufanya uovu machoni pa Yahwe Mungu wenu, kumchoche katika hasira- \v 26 Nitaita nchi na mbingu kushuhudia dhidi yenu leo kwa kuwa mapema kabisa mtaangamia kutoka katika nchi ambayo mnaiendea huko ng'ambo ya Yordani kuimiliki, hamtazidisha siku zenu ndani yake, lakini mtaangamizwa kabisa.

1
04/27.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 27 Yahwe atawatawanyisha ninyi miongoni mwa watu, na mtabaki wachache ki-idadi miongoni mwa mataifa, ambapo Yahwe atawaongoza mbali. \v 28 Huko mtatumikia miungu mingine, kazi ya mikono ya watu, mbao na mawe, ambayo wala haioni, kusikia, wala kunusa.

1
04/29.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 29 Lakini kuanzia hapo mtamtafuta Yahwe Mungu wenu, na mtampata, wakati mtakapomtafuta kwa moyo wenu wote na roho zenu zote.

1
04/30.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 30 Wakati mnakuwa katika dhiki, na wakati haya yote yatakuwa yamekuja kwenu, katika siku za badae mtamrudia Yahwe Mungu wenu na kusikia sauti yake. \v 31 Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ni Mungu wa rehema; hatawaangusha wala kuwaangamiza ninyi, wala kusahau agano la baba zenu ambalo aliapa kwao.

1
04/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 Kwa ajili ya kuuliza sasa kuhusu siku zilizopita ambazo zilikuwa mbele yenu: tangu siku ile ambayo Mungu alimuumba mtu katika nchi, kutoka pande moja ya mbingu hadi nyingine, uliza kama kumekuwepo chochote kama hiki kikubwa, au chochote kama hicho imewahi kusikiwa? \v 33 Ilishawahi kutokea watu kusikia sauti ya Mungu kuongea katikati ya moto, kama mlivyosikia, na kuishi?

1
04/34.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 34 Au Mungu ameshawahi kujaribu kwenda na kujichukulia kwa ajili yake taifa kutoka miongoni mwa taifa, kwa majaribu, ishara na maajabu na kwa vita, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoshwa, na magaidi wakuu, vile vyovyote ambavyo Yahwe Mungu wenu alifanya kwa ajili yenu Misri mbele ya macho yenu?

1
04/35.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 35 Kwenu haya yalioneshwa, ili muweze kujua kuwa Yahwe ni Mungu, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake. \v 36 Toka mbinguni alifanya msikie sauti yake, ili kwamba aweze kuwaelekeza, juu ya nchi aliwafanya muone moto wake mkuu, mlisikia maneno yake toka katikati ya moto.

1
04/37.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 37 Kwa sababu aliwapenda baba zenu, alichagua wazao wao baada yao, na kuwatoa ninyi Misri kwa uwepo wake, kwa nguvu yake kubwa, \v 38 ili kusudi awatowe kutoka mbele ya mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi, kuwaleta ndani, kuwapa ninyi nchi yao kama urithi, hivi leo.

1
04/39.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 39 Tambua hivi leo, weka kwenye moyo wako, Yahwe ni Mungu juu ya mbingu na chini ya dunia, hakuna mwingine yeyote. \v 40 Mtazishika sheria zake na amri zake ambazo nawaamuru leo, ili kwamba iweze kuwa vizuri kwenu na watoto wenu baada yenu, na kwamba muweze kuongeza siku zenu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu amewapa milele."

1
04/41.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 41 Kisha Musa alichagua miji mitatu mashariki mwa Yordani, \v 42 ili kwamba yoyote aweze kukimbia kati ya moja yao kama imemuua mtu mwingine kwa ajili, pasipo kuwa adui hapo awali. Kwa kukimbilia kwenye moja ya miji hii, atakuwa amenusurika. \v 43 Walikuwa: Bezeri katika jangwa, nchi tambarare, kwa Warubenites; Ramothi huko Gileadi, kwa Gadites; na Golani huko Bashani, kwa Manassites.

1
04/44.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 44 Hii ni sheria ambayo Musa aliweka mbele ya watu wa Israeli, \v 45 hizi ni amri za agano, sheria, na amri zingine alizungumza na watu wa Israeli wakati walipotoka Misri, \v 46 pindi walikuwa Mashariki mwa Yordani, katika bonde mkabala wa Beth Peori, katika nchi ya Sihoni, mfalme wa Amorites, aliyewahi kuishi Heshbon, ambaye Musa na watu wa Israeli waliwahi kumshinda wakati walipotoka Misri.

1
04/47.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 47 Walichukua nchi yake kama urithi, na nchi ya Ogi mfalme wa Bashani- hawa, wafalme wawili wa Amorites, waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani kuelekea Mashariki. \v 48 Himaya hii ilienda kutoka Aroer, katika ukingo wa bonde la Arnon, kwa mlima wa Sion (mlima Hermon), \v 49 na ilijumuisha tambarare zote za bonde la mto Yordani, Mashariki mwa ng'ambo ya pili ya Yordani, kuelekea bahari ya Arabah, kuelekea miteremko ya mlima Pisgah.

1
05/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Musa aliwaita Israeli yote na akasema nao, "Sikiliza, Israeli, kwa amri na sheria ambazo nitasema katika masikio yenu leo, muweze kujifunza na kuzishika. \v 2 Yahwe Mungu wetu alifanya agano nasi huko Horeb. \v 3 Yahwe hakufanya agano hili pamoja na mababu zetu, lakini na sisi, sisi wote tu hai hapa leo.

1
05/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Yahwe alizungumza nawe uso kwa uso kwenye mlima toka katikati mwa moto \v 5 (Nilisimama kati ya Yahwe na wewe kwa wakati huo, kukufunulia wewe neno lake, kwa kuwa ulikuwa umeogopa kwa sababu ya moto, na haukwenda juu ya mlima), Yahwe alisema, \v 6 'Mimi ni Yahweh Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa.

1
05/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Hautakuwa na miungu mingine mbele yangu. \v 8 Hautajifanyia mwenyewe sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini ya dunia, au kilicho chini ya maji.

1
05/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Hautavisujudia au kuvitumikia, kwa kuwa Mimi, Yahwe Mungu wako, ni Mungu wa wivu, Nawaadhibu uovu wa mababu kwa kuleta adhabu juu ya watoto, kwa kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanichukiao, \v 10 na kuonesha agano la uaminifu kwa maelfu, kwa wale wanaonipenda na kushika amri zangu.

1
05/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Hautalichukua jina la Yahwe Mungu wako bure, kwa kuwa Yahwe hatamshikilia kuwa ana hatia yeye alichukuae jina bure.

1
05/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Zingantia siku ya Sabato kwa kuiweka takatifu, kama Yahwe Mungu wako alivyokuamuru. \v 13 Kwa siku sita utafanya kazi na fanya kazi zako zote, \v 14 lakini siku ya saba ni Sabato kwa Yahwe Mungu wako. Kwa siku hiyo hautafanya kazi yoyote- si wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mjakazi wako wa kiume, wala maksai wako, wala punda wako, wala mifugo wako, wala mgeni yeyote aliye katika malango yako. Hii ni kwamba mjakazi wako wa kiume na mjakazi wako wa kike wapate kumpuzika pamoja na wewe.

1
05/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Utakumbuka katika akili yako kwamba ulikuo mtumwa katika nchi ya Misri, na Yahwe Mungu wako alikutoa kutoka huko kwa mkono wa uweza na mkono ulionyoshwa. Kwa hiyo Yahwe Mungu wako amekuamuru kuitunza siku ya Sabato.

1
05/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Mheshimu baba yako na mama yako, kama Yahwe Mungu wako alivyokuamuru kufanya, ili kwamba uweze kuishi muda mrefu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako akupa, ili kwamba iende kwa uzuri kwako.

1
05/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Hautaua, \v 18 hautazini, \v 19 hautaiba, \v 20 hautashuhudia uongo dhidi ya ndugu yako.

1
05/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Hautamtamani mke wa jirani yako, hautatamani nyumba ya jirani yako, shamba lake, au mjakazi wake wa kiume, au mjakazi wake wa kike, maksai au punda wako, au chochote ambacho ni mali ya jirani yako.

1
05/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Haya maneno Yahwe alisema kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lako lote kwenye mlima toka katikati mwa moto, mawingu, giza zito, hakuongeza maneno yoyote zaidi. Na aliandika chini kwenye mbao mbili za mawe na akanipa mimi.

1
05/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Ilipokaribia, pindi uliposikia sauti toka katikati mwa giza, wakati mlima unawaka moto, kuwa mlikuja karibu nami, wazee wako wote, na wakuu wa makibila yako. \v 24 Ulisema, Tazama, Yahwe Mungu wetu ametuonesha utukufu wake na ukuu wake, na tumeisikia sauti yake toka katikati mwa moto, tumeona leo kwamba wakati Mungu azungumza na watu, wanaweza kuishi.

1
05/25.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 25 Lakini kwanini tufe? Kwa kuwa mto huu mkuu utatutoshereza sisi; kama tutasikia sauti ya Yahwe Mungu wetu tena, tutakufa. \v 26 Kwa kuwa badala yetu kuna miongoni mwetu wa mwili ambao wamesikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza toka katikati mwa moto na kuishi, kama tulivyofanya? \v 27 Kwenu ninyi, mnapaswa kwenda na kusikiliza kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema; rudia kwetu kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema kwenu; tutamsikiliza na kumtii.'

1
05/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Yahweh alisikia maneno yenu pindi mlipozungumza nami. Alisema na mimi, "Nimekwisha sikia maneno ya watu hawa, kile wanasema kwako. Kile walichosema kilikuwa kizuri. \v 29 Oh, kulikuwa na moyo wa namba hiyo ndani yao, kwamba wataniheshimu na daima kushika amri zangu zote, ili iweze kuwa vizuri kwao na pamoja na watoto wao milele! \v 30 Nenda useme nao, "Rudini kwenye mahema."

1
05/31.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 31 Lakini kwenu, simama karibu nami, na nitakuambia amri zote, sheria, na maagizo ambayo mtawafundisha, ili kwamba waweze kuyashika katika nchi ambayo nitawapa kumiliki.'

1
05/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 Utashika, kwa hiyo, kile Yahwe Mungu wenu amewaamuru; hamtageukia mkono wa kulia au kushoto. \v 33 Mtatembea katika njia zote ambazo Yahwe Mungu wenu, amewaamuru ili kusudi muweze kuishi, na ili kwamba iweze kwenda vizuri kwenu, na kwamba muweze kuongeza siku zenu katika nchi ambayo mtaimiliki.

1
06/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Sasa haya ni maagizo, amri, na sheria ambazo Yahwe Mungu wetu ameniamuru mimi kuwafundisha ninyi, ili kwamba muweze kuzishika katika nchi ambayo mnaenda ng'ambo ya pili ya Yordani kumiliki, \v 2 ili kwamba mpate kumheshimu Yahwe wenu, ili muzishike amri zake zote na maagizo ninayowaamuru-ninyi, wana wenu na wana wa wana wenu, siku zenu zote za maisha, ili kwamba siku zenu ziongezeke.

1
06/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Kwa hiyo wasikilizeni, Israeli, na kuzishika ili kwamba iweze kuwa vizuri kwenu, ili kusudi muweze kuzidi mno kwenye nchi itiririkayo maziwa na asali, kama Yahwe Mungu wa Baba zenu, amewaahidi atafanya.

1
06/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Sikiliza, Israel: Yahwe Mungu wetu ni mmoja. \v 5 Mtampenda Yahwe Mungu wenu kwa moyo wenu wote, kwa roho zenu zote, na kwa akili zenu zote.

1
06/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Maneno ninayowaamuru ninyi leo yatakuwa katika moyo wenu; \v 7 na mtayafundisha kwa bidii kwa watoto wenu, mtayazungumza wakati mkaapo katika nyumba zenu, wakati mlalapo, na wakati mwinukapo.

1
06/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Utazifunga kama ishara juu ya mkono wako, nayo yatakuwa utepe kati ya macho yako. \v 9 Utaziandika kwenye miimo ya mlango ya nyumba yako na kwenye malango.

1
06/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Wakati Yahwe Mungu wako akuleta kwenye nchi ambayo aliaapa kwa baba zako, Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, kwamba angekupa, pamoja na miji mikubwa na mizuri ambayo hamkuijenga, \v 11 na nyumba zilizojaa kila aina ya vitu vizuri ambavyo hamkuzifanya, visima ambavyo hamkuvichimba, mashamba na miti ya mizeituni ambayo hamkuipanda, mtakula na kutosheka- \v 12 basi iweni makini ili kwamba msije kumsahau Yahwe, aliyewaleta toka nchi ya Misri, toka nyumba ya utumwa.

1
06/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Mtamheshimu Yahwe Mungu wenu, yeye mtamwabudu, na mtaapa kwa jina lake. \v 14 Hamtawaendea miungu mingine, miungu ya watu wanaowazunguka wote- \v 15 kwa kuwa Yahwe Mungu wenu katikati yenu ni Mungu wa wivu- kama mtafanya, hasira ya Yahwe Mungu wenu atawasha dhidi yenu na atawaangamiza kutoka kwenye uso wa dunia.

Some files were not shown because too many files have changed in this diff Show More