sw_dan_text_reg/09/03.txt

1 line
388 B
Plaintext

\v 3 Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu, ili kumtafuta yeye kwa sala na maombi, kwa kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu. \v 4 Nilimwomba Yahweh Mungu wangu, na niliungama dhambi zetu. Nilisema, "Tafadhali, Bwana, wewe ni Mungu mkuu na mwenye kuheshimiwa, wewe hutunza maagano na uliye mwaminifu katika kuwapenda wale wanaokupenda wewe na kuzishika amri zako.