sw_dan_text_reg/06/06.txt

1 line
457 B
Plaintext

\v 6 Ndipo watawala hawa na magavana walileta mpango mbele ya mfalme. Walimwambia, "Mfalme Dario, uishi milele! \v 7 Watawala wote wakuu wa ufalme, magavana wa mikoa, na magavana wa majimbo, washauri, na magavana wameshauriana kwa pamoja na kuamua kuwa wewe, mfalme, unapaswa kupitisha amri na kuitekeleza, ili kwamba mtu yeyote anayefanya dua kwa mungu yeyote au mtu kwa siku thelathini, isipokuwa wewe mfalme, mtu huyo lazima atupwe katika tundu la simba.