sw_dan_text_reg/06/01.txt

1 line
462 B
Plaintext

\v 1 Ilimpendeza Dario kuchagua juu ya ufalme magavana wa majimbo 120 ambao wangetawala juu ya ufalme wote. \v 2 Juu yao kulikuwa na watawala wakuu watatu, na Daniel alikuwa mmoja wao. Hawa watawala waliwekwa ili waweze kuwasimamia magavana wa majimbo, ili kwamba mfalme asipate hasara. \v 3 Danieli alipambanuliwa juu ya watawala wakuu na juu ya magavana wa majimbo kwasababu alikuwa na roho isiyo ya kawaida. Mfalme alikuwa akipanga kumweka juu ya ufalme wote.