sw_dan_text_reg/03/03.txt

1 line
563 B
Plaintext

\v 3 Ndipo magavana wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na washauri, wahasibu, waamuzi, mahakimu, na maafisa wa juu wa majimbo walikusanyika kwa pamoja katika uzinduzi wa sanamu ambayo Nebukadneza aliyokuwa ameiweka. Walisimama mbele yake. \v 4 Kisha mtangazaji alipiga kelele, "Enyi watu, mataifa, na lugha mmeamriwa \v 5 kwamba mtakaposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, ni sharti kuanguka na kuisujudia ninyi wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameiweka.