sw_dan_text_reg/01/19.txt

1 line
457 B
Plaintext

\v 19 Mfalme aliongea nao, na miongoni mwa kundi lote hapo hapakuwa na wa kuwalinganisha na akina Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria. Walisimama mbele ya mfalme, wakiwa tayari kumtumikia. \v 20 Katika kila swali la hekima na ufahamu ambalo mfalme aliwauliza, aliwakuta wakiwa na uwezo mara kumi kuliko waganga wote na wale waliojidai kusema na wafu, waliokuwa katika ufalme wake wote. \v 21 Danieli alikuwepo hapo mpaka mwaka wa kwanza wa Mfalme Koreshi.