sw_dan_text_reg/02/36.txt

1 line
391 B
Plaintext

\v 36 Hii ndiyo ilikuwa ndoto yako. Na sasa tutamwambia mfalme maana yake. \v 37 Wewe, mfalme, ni mfalme wa wafalme kwa wale ambao Mungu wa mbinguni amewapa ufalme, nguvu, uweza na heshima. \v 38 Ametia mkononi mwako sehemu ambazo binadamu huishi. Amekupa wanyama wa mwituni na ndege wa angani katika mkono wako, na amekufanya wewe utawale juu yao wote. Wewe u kichwa cha dhahabu cha sanamu.