sw_dan_text_reg/02/34.txt

1 line
468 B
Plaintext

\v 34 Ulitazama juu, na jiwe lilikuwa limechongwa, ingawa si kwa mikono ya wanadamu, na liliipiga sanamu katika miguu yake ya chuma na udongo, na kuiponda ponda. \v 35 Kisha chuma, udongo, fedha, na dhahabu zilivunjwa katika vipande vipande kwa wakati mmoja na yakawa kama makapi yaliyo katika sakafu za kupuria kipindi cha kiangazi. Upepo ukayapeperushia mbali na hakuna alama yake iliyoachwa. Lakini jiwe lililoipiga sanamu likawa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.