sw_dan_text_reg/12/03.txt

1 line
320 B
Plaintext

\v 3 Wale wenye hekima watang'ara kama mng'ao wa anga la juu, na wale wenye kuwaelekeza wengine katika haki, watakuwa kama nyota milele na milele. \v 4 Lakini wewe, Danieli, yafunge maneno haya; kihifadhi kitabu kikiwa kimetiwa muhuri mpaka nyakati za mwisho. Watu wengi watakimbia huku na kule, na maarifa yataongezeka.