sw_dan_text_reg/11/36.txt

1 line
429 B
Plaintext

\v 36 Mfalme atafanya kutokana na matakwa yake. Atajiinua mwenyewe na kujifanya mkubwa kuliko kila muungu. Kinyume cha Mungu wa miungu, atasema vitu vibaya, kwa kuwa atafanikiwa mpaka pale ghadhabu itakapokuwa imekamilika. Kwani kile kilichokuwa kimeamriwa kitafanyika. \v 37 Hataijali miungu ya baba zake wala muungu anayependwa na wanawake, hata muungu mwingine yeyote hatamjali, lakini atajitukuza mwenyewe juu ya miungu yote.