sw_dan_text_reg/11/25.txt

1 line
590 B
Plaintext

\v 25 Ataamsha nguvu zake na moyo wake kinyume na mfalme wa Kusini kwa jeshi kubwa. Mfalme wa Kusini atapigana vita akiwa na jeshi kubwa hasa na lenye nguvu, lakini hataweza kusimama kwa kuwa wengine watafanya njama dhidi yake. \v 26 Hata wale wanaokula chakula chake kizuri watajaribu kumwangamiza. Jeshi lake litakatiliwa mbali kama gharika, na wengi wao watauawa. \v 27 Wafalme wote hawa wawili, wakiwa na mioyo yao imejawa na uovu kinyume na mwenzake, watakaa katika meza moja na kudanganyana, lakini haitakuwa na maana yoyote. Kwa kuwa mwisho utatokea kwa wakati uliokwisha kupangwa.