sw_dan_text_reg/11/17.txt

1 line
585 B
Plaintext

\v 17 Mfalme wa Kaskazini atauelekeza uso wake ili kuja kwa nguvu za ufalme wake wote, na kutakuwa na makubaliano atakayoyafanya na mfalme wa Kusini. Atampatia katika ndoa binti wa wanawake ili kuuharibu ufalme wa Kusini. Lakini mpango huo hautafanikiwa wala kumsaidia. \v 18 Baada ya hili, mfalme Kaskazini atakazia macho nchi za pwani na ataziteka nyingi kati ya hizo. Lakini amiri jeshi atakikomesha kiburi chake na atakisababisha kiburi chake kimgeuke mwenyewe. \v 19 Kisha atafuatilia miji yenye ngome katika nchi yake mwenyewe, lakini atajikwaa na kuanguka; na hatapatikana tena.