sw_dan_text_reg/11/15.txt

1 line
383 B
Plaintext

\v 15 Mfalme wa Kaskazini atakuja, kuizingira nchi kwa kuweka vilima, na kuuteka mji wenye ngome. Majeshi ya Kusini hayataweza kusimama, hata wanajeshi wake bora. Hawatakuwa na nguvu za kusimama. \v 16 Badala yake, yeye ajaye dhidi yake ataenenda kama atakavyo, na hakuna hata mmoja atakayesimama katika njia yake. Atasimama katika Nchi ya Uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.