sw_dan_text_reg/10/12.txt

1 line
385 B
Plaintext

\v 12 Kisha aliniambia, "Usiogope, Danieli. Tangu siku ya kwanza ulipoiweka akili yako kutaka kufahamu na kujinyenyekeza mwenyewe mbele ya Mungu, maneno yako yalisikiwa, na nimekuja kwasababu ya maneno yako. \v 13 Mwana wa mfalme wa ufalme wa Uajemi alinipinga, na nilizuiliwa huko na wafalme wa Uajemi kwa siku ishirini na moja. Lakini Mikaeli, mmoja kati ya wakuu alikuja kunisaidia.