sw_dan_text_reg/09/09.txt

1 line
406 B
Plaintext

\v 9 Kwa Bwana Mungu wetu kuna huruma na msamaha, kwa kuwa tumemwasi yeye. \v 10 Hatujaitii sauti ya Yahweh Mungu wetu kwa kutembea katika sheria zake alizotupatia kupitia watumishi wake manabii. \v 11 Israeli wote wameiasi sheria yako na kugeukia upande, kwa kukataa kuitii sauti yako. Laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu, vimemwagwa juu yetu kwa kuwa tumemtenda dhambi.