sw_dan_text_reg/08/15.txt

1 line
453 B
Plaintext

\v 15 Wakati mimi Danieli, nilipoona maono, nilijaribu kuyaelewa. Ndipo mbele yangu alisimama yule aliyeoneakana kama mtu. \v 16 Niliisikia sauti ya mtu ikiita katikati ya kingo za mfereji wa Ulai. Alisema, "Gabrieli, msaidie mtu huyu kuelewa maono." \v 17 Basi alikuja karibu na mahali niliposimama. Na alipokuja, nilishtuka na nikaanguka kifudifudi hadi chini. Lakini aliniambia, "Fahamu, mwana wa mtu, kwamba maono ni kwa ajili ya wakati wa mwisho."