sw_dan_text_reg/08/07.txt

1 line
499 B
Plaintext

\v 7 Niliiona mbuzi akija karibu na kondoo. Mbuzi alikuwa na hasira kali dhidi ya kondoo, na alimgonga kondoo na kuzivunja pembe zake mbili. Kondoo hakuwa na nguvu za kusimama mbele zake. Mbuzi alimgonga kondoo kwa kumbwaga chini na kumkanyagakanyaga. Hapakuwa na yeyote wa kumwokoa kutoka katika nguvu zake. \v 8 Ndipo mbuzi alikua mkubwa sana, lakini alipokuwa na nguvu, pembe kubwa ilivunjwa, na katika sehemu yake zilichipuka na kukua pembe nne kubwa zilizochomoza kuelekea pepo nne za mbingu.