sw_dan_text_reg/07/19.txt

1 line
557 B
Plaintext

\v 19 Ndipo nilipotaka kujua zaidi juu ya mnyama wa nne, ambaye alikuwa tofauti sana na wengine na alikuwa wa kutisha pamoja na meno yake ya chuma na makucha ya shaba; alimeza, na alivunja vipande vipande, na alisagasaga kwa miguu yake kile kilichokuwa kimesalia. \v 20 Nilitaka kujua juu ya pembe kumi katika kichwa chake, na kuhusu pembe nyingine iliyochomoza, na ambayo mbele yake pembe nyingine tatu zilianguka chini. Nilitaka kujua kuhusu pembe yenye macho na kuhusu mdomo uliojigamba kwa mambo makuu na ambayo ilionekana kuwa ni kubwa kuliko nyingine.