sw_dan_text_reg/05/22.txt

1 line
600 B
Plaintext

\v 22 Wewe mwana wake, Belshaza, haujaunyenyekeza moyo wako, ingawa uliyajua haya yote. \v 23 Umejiinua mwenyewe kinyume cha Bwana wa mbinguni. Katika nyumba yake walikuletea vyombo ambavyo wewe, wakuu wako, wake zako na masuria wako walivinywea, na kisha ukaisifia sana sanamu zilitengenezwa kwa fedha na dhahabu, shaba, chuma, mbao, na mawe--sanamu ambazo haziwezi kuona, kusikia wala kujua kitu chochote. Haujamheshimu Mungu ambaye anaishikilia pumzi yako katika mkono wake na ambaye anazijua njia zako zote. \v 24 Ndipo Mungu aliutuma mkono kutoka katika makao yake na maandishi haya yaliandikwa.