sw_dan_text_reg/05/20.txt

1 line
493 B
Plaintext

\v 20 Lakini moyo wake ulipokuwa na kiburi na roho yake ilipofanywa kuwa ngumu kiasi cha kutenda kwa kiburi, alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme, na waliiondoa enzi yake. \v 21 Aliondolewa mbali na ubinadamu, akawa na akili za mnyama, na akaishi na punda wa mwituni. Alikula majani kama ng'ombe. Mwili wake ulilowanishwa kwa umande wa kutoka mbinguni mpaka pale alipojifunza kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na ya kwamba humweka mtu yeyote amtakaye juu yake.