sw_dan_text_reg/05/17.txt

1 line
530 B
Plaintext

\v 17 Kisha Danieli akajibu mbele ya mfalme, "Zawadi zako na ziwe kwa ajili yako mwenyewe, na thawabu zako umpe mtu mwingine. Hata hivyo, mfalme, nitakusomea maandishi na nitakwambia maana. \v 18 Na juu yako, Ewe mfalme, Mungu Aliye juu sana alimpa Nebukadneza baba yako ufalme, ukuu, heshima na enzi. \v 19 Na kwasababu ya ukuu huo, Mungu alimpa watu wote, mataifa, na lugha walimtetemekea na kumwogopa. Aliwauwa wale aliotaka wafe na aliwaacha hai wale aliotaka waishi. Aliwainua wale aliowataka, na aliwashusha wale aliowataka.