sw_dan_text_reg/04/36.txt

1 line
488 B
Plaintext

\v 36 Kwa wakati ule ule utimamu wa akili zangu uliponirudia, utukufu wangu na fahari yangu ilinirudia kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na watu wenye heshima walitafuta msaada wangu. Nilirudishwa kwenye kiti changu cha enzi, na nilipewa ukuu zaidi. \v 37 Sasa basi, mimi Nebukadneza, ninamsifu, ninamtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni, kwa kuwa matendo yake yote ni ya haki, na njia zake ni za haki. Anaweza kuwashusha wale wanaotembea katika kiburi chao wenyewe.