sw_dan_text_reg/04/24.txt

1 line
452 B
Plaintext

\v 24 Mfalme, hii ni tafsiri yake. Ni agizo la Yeye Aliye Juu ambalo limekufikia, bwana wangu mfalme. \v 25 Utafukuzwa utoke miongoni mwa watu, na utaishi pamoja na wanyama wa mwituni huko mashambani. Utafanywa uwe unakula majani kama ng'ombe, na utalowanishwa na umande wa kutoka mbinguni, miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme zote za watu na ya kwamba yeye huwapa hizo falme kwa mtu yeyote amtakaye.