sw_dan_text_reg/04/15.txt

1 line
336 B
Plaintext

\v 15 Mkiache kisiki cha mizizi yake katika nchi, mkifunge na fungu la chuma na shaba, katikati ya mche mororo wa shambani. Na kilowanishwe na umande wa kutoka mbinguni. Kiacheni kiishi na wanyama kati ya mimea ya ardhini. \v 16 Acha akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba.