sw_dan_text_reg/04/10.txt

1 line
563 B
Plaintext

\v 10 Haya ndiyo niliyoyaona katika akili zangu nilipokuwa nimejilaza katika kitanda changu: Nilitazama, na kulikuwa na mti katikati ya dunia, na urefu wake ulikuwa ni mkubwa sana. \v 11 Mti ulikua na ukawa wenye nguvu. Na sehemu ya juu yake ilifika mbinguni, uliweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote. \v 12 Majani yake yalikuwa mazuri, matunda yake yalikuwa ni mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Wanyama wa mwituni walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani waliishi katika matawi yake. Viumbe vyote hai vililishwa katika mti huo.