sw_dan_text_reg/04/07.txt

1 line
536 B
Plaintext

\v 7 Kisha walikuja wachawi, wale ambao hudai kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wasoma nyota. Niliwaambia juu ya ndoto, lakini hawakuweza kunitafsiria. \v 8 Bali mwishoni Danieli aliingia ndani--yeye ambaye huitwa Belteshaza jina la muungu wangu, na ambaye ndani yake kuna roho ya miungu mitakatifu--na nilimwambia juu ya ndoto. \v 9 "Belteshaza, mkuu wa wachawi, ninajua kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako na ya kwamba hakuna siri iliyo ngumu kwako. Niambie kile nilichokiona katika ndoto yangu na nini tafsiri yake.