sw_dan_text_reg/04/01.txt

1 line
408 B
Plaintext

\c 4 \v 1 Mfalme Nebukadneza aliituma amri hii kwa watu wote, mataifa, na lugha walioishi katika nchi: "Na amani yenu na iongezeke. \v 2 Imeonekana vyema kwangu kuwaambia juu ya ishara na maajabu ambayo Mungu Mkuu Aliye juu amenifanyia. \v 3 Ni kwa namna gani Ishara zake ni kuu, na ni kwa namna gani maajabu yake yana nguvu! Ufalme wake ni ufalme unaodumu milele, na utawala wake hudumu kizazi hadi kizazi."