sw_dan_text_reg/03/06.txt

1 line
320 B
Plaintext

\v 6 Na yeyote asiyeanguka na kuiabuda, kwa wakati huo huo atatupwa katika tanuru la moto." \v 7 Basi watu waliposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, watu wote, mataifa na lugha walianguka na kuisujudia sanamu ya dhahabu ambayo Nebukadneza mfalme alikuwa ameiweka.