sw_act_text_ulb/19/30.txt

1 line
411 B
Plaintext

\v 30 Paulo alitaka kuingia katika umati wa watu, lakini wanafunzi walimzuia. \v 31 Pia, baadhi ya maafisa wa mkoa wa Asia ambao walikuwa marafiki zake wakampelekea ujumbe kwa nguvu kumwomba asiingie katika ukumbi wa michezo. \v 32 Baadhi ya watu walikuwa wakipiga kelele jambo moja na wengine lingine, kwa sababu umati wa watu ulikuwa umechanganyikiwa. Wengi wao hawakuweza hata kujua kwa nini walikuja pamoja.