sw_act_text_ulb/21/05.txt

1 line
286 B
Plaintext

\v 5 Wakati siku zetu zilipoisha, tuliondoka tukaenda zetu, na wao wote pia, wakiwa na wake na watoto wao, walitusindikiza katika njia hadi tulipotoka nje ya mji. Kisha tukapiga magoti pwani, tukaomba, tukaagana kila mmoja. \v 6 Ndipo tulipanda meli tena, na wao wakarudi nyumbani kwao.