sw_act_text_ulb/15/36.txt

1 line
346 B
Plaintext

\v 36 Baada ya siku kadhaa Paulo alisema kwa Barnaba, "Na turudi sasa na kuwatembelea ndugu katika kila mji tulipohubiri neno la Bwana, na kuwaona walivyo. \v 37 Barnaba alihitaji pia kumchukua pamoja na Yohana aliyeitwa Marko. \v 38 Lakini Paulo alifikiri haikuwa vizuri kumchukua Marko, aliyewaacha huko Pamfilia na hakuendelea nao katika kazi.