sw_act_text_ulb/14/11.txt

1 line
399 B
Plaintext

\v 11 Umati ulipoona alichokifanya Paulo, waliinua sauti zao, wakisema katika lahaja ya Kilikaonio, "miungu imekuwa kama wanadamu na imeshuka kwetu." \v 12 Walimwita Barnaba "Zeu," na Paulo "Herme" kwa sababu alikuwa msemaji mkuu. \v 13 Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje ya mji, alileta fahari la ng'ombe na mtungo wa maua mpaka kwenye lango la mji, yeye na umati walitaka kutoa sadaka.